Jumamosi 20 Septemba 2025 - 21:34
Kuingizwa jina la “Kataib Sayyid al-Shuhada” katika orodha ya magaidi na Marekani ni alama ya fahkari kwetu

Hawzah/ Abu Ala al-Wala’i, Katibu Mkuu wa Kataib Sayyid al-Shuhada, akijibu kuingizwa kwake na “Kataib Sayyid al-Shuhada” kwenye orodha ya magaidi na Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani, ameona hatua hiyo kuwa haina umuhimu, na ameielezea kama chanzo cha fakhari na alama ya nafasi na heshima ya kundi analoliongoza.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Abu Ala al-Wala’i, Katibu Mkuu wa Kataib Sayyid al-Shuhada, katika ujumbe aliouandika kwenye mtandao wa kijamii X (Twitter ya zamani) aliandika hivi: “Habari iliyotuorodhesha katika magaidi haina thamani yoyote; bali imeongeza heshima na nafasi yetu.”

Al-Wala’i pia, akirejea tukio la mlipuko wa “pager” uliotokea mwaka jana kusini mwa Lebanon, aliwakumbuka wahanga wa tukio hilo kama “mashujaa” na kwa maneno yenye hisia aliwahutubia wapiganaji wa Hizbullah kwa kusema: “Tunabusu macho na mikono yenu ambayo kwa hayo mlimliwaza Abul-Fadhl al-Abbas (a.s.).”

Kauli hizi za Katibu Mkuu wa Kataib Sayyid al-Shuhada zinakuja kuijibu Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani, ambayo imeweka jina la kikosi hicho kwenye orodha ya makundi ya kigaidi kwa madai ya “kutishia amani na uthabiti wa Iraq” na “kuhusika na vitendo vya kigaidi.”

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha